Mhashamu Sana na Mheshimiwa Sana Dame Sarah Mullally DBE kuwa Askofu Mkuu wa Canterbury wa 106

AB Sarah 1920x 1080

Mfalme Mkuu ameidhinisha uteuzi wa Askofu wa London, Mhashamu Sana na Mheshimiwa Sana Dame Sarah Mullally, kuwa Askofu Mkuu ajaye wa Canterbury, Ofisi ya Waziri Mkuu imetangaza.

Askofu Mkuu wa Canterbury wa 106 tangu Mtakatifu Augustine alipowasili Kent kutoka Roma mwaka 597, Askofu Sarah atakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.

Atasimikwa katika ibada itakayofanyika katika Kanisa Kuu la Canterbury mnamo Machi 2026.  

Sarah Mullally amekuwa Askofu wa London tangu mwaka 2018, mwanamke wa kwanza kuteuliwa kwenye jukumu hilo, na kabla ya hapo alikuwa Askofu wa Crediton katika Dayosisi ya Exeter. Kabla ya kutawazwa kwake mwaka 2001, alikuwa Afisa Mkuu wa Uuguzi wa Serikali ya Uingereza, mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuteuliwa kwenye jukumu hilo akiwa na umri wa miaka 37, akiwa amewahi kuwa muuguzi wa saratani hapo awali. Askofu Sara ameelezea uuguzi kama "fursa ya kuonyesha upendo wa Mungu".

Tume ya Uteuzi ya Mfalme (CNC) ya Canterbury ilimteua Askofu Sarah kufuatia mchakato wa mashauriano ya umma na utambuzi kupitia maombi ambao ulianza Februari mwaka huu. Canterbury CNC iliundwa na wawakilishi kutoka Kanisa lote la Uingereza, Ushirika wa Anglikana duniani na Dayosisi ya Canterbury.

Askofu mwandamizi zaidi katika Kanisa la Uingereza, huduma ya Askofu Mkuu wa Canterbury inahusisha majukumu mengi ikiwa ni pamoja na kutumikia kama Askofu wa Dayosisi ya Canterbury, Askofu Mkuu wa Uingereza yote na Metropolitan, pamoja na primus inter pares, au wa kwanza kati ya wanaolingana, wa Wakuu wa Ushirika wa Anglikana ulimwenguni, ambao una watu wapatao milioni 85, katika nchi 165. Katika Baraza la Wakuu, Askofu Mkuu wa Canterbury ni mmoja wa maaskofu 26 ambao wanajumuisha Wakuu wa Kiroho. 

Askofu Sarah alisema: “Ninapoitikia wito wa Kristo katika huduma hii mpya, ninafanya hivyo kwa roho ile ile ya kumtumikia Mungu na kuwatumikia wengine ambayo imenihamasisha tangu nilipokuwa kijana.

"Katika kila hatua ya safari hiyo, kupitia kazi yangu ya uuguzi na huduma ya Kikristo, nimejifunza kusikiliza kwa kina, kuwasililiza watu na sauti ya upole ya Mungu, kutafuta kuwaleta watu pamoja ili kupata tumaini na uponyaji.

"Ninachotaka tu ni kulihimiza Kanisa kuendelea kukua katika ujasiri katika Injili, kuzungumzia upendo ambao tunapata katika Yesu Kristo na ili uweze kuongoza matendo yetu.

"Na ninatazamia kusafiri pamoja safari hii ya imani na mamilioni ya watu wanaomtumikia Mungu na jamii zao katika parokia kote nchini na katika Ushirika wa Anglikana ulimwenguni.

"Najua hili ni jukumu kubwa lakini ninalichukulia nikiwa na amani na kumwamini Mungu kunibeba kama alivyofanya siku zote."

Mheshimiwa Evans, Mwenyekiti wa Tume ya Uteuzi ya Mfalme ya Canterbury, alisema: "Imekuwa fursa kubwa kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uteuzi ya Mfalme kwa kuwa ilitafuta kutambua ni nani Mungu anamwita kuongoza Kanisa la Uingereza na Ushirika wa Anglikana kama Askofu Mkuu wa Canterbury. Utambuzi huo ulianza kwa mashauriano ya umma, ambayo yalisikia sauti za maelfu ya watu walipoelezea matumaini yao kuhusu uteuzi huu, na kuendelea hadi kikao cha mwisho cha Tume. Ningependa kuwashukuru wale wote walioshiriki katika mchakato huu, hasa wale ambao walichukua muda wa kutoa maoni yao katika mashauriano na wajumbe wa Tume ambao walifanya kazi kwa bidii kwa miezi kadhaa, wakisaidiwa na Makatibu wa Uteuzi na timu ya Uteuzi na Miito katika Lambeth Palace. Nitakuwa nikimwombea Askofu Sarah wakati anajiandaa kutekeleza huduma hii mpya katika miezi ijayo.”   

Askofu Anthony Poggo, Katibu Mkuu wa Ushirika wa Anglikana, alisema: "Ninapokea na kupongeza uteuzi wa Askofu Sarah kuwa Askofu Mkuu ajaye wa Canterbury na kuyaalika makanisa ya Ushirika wa Anglikana ulimwenguni kumuombea anapojiandaa kutekeleza huduma hii muhimu. Mungu ampe hekima na utambuzi, anapotafuta kusikiliza makanisa Washirika, kuhimiza kusaidiana, na kukuza umoja.

"Ofisi ya Ushirika wa Anglikana imejitolea kikamilifu kusaidia huduma yake anapofanya kazi na Majimbo mengine na Vyombo vya Ushirika wa Anglikana. Tuombe kwamba Mungu amimine Roho wake kwenye Ushirika wa Anglikana ili kushiriki kwa ujasiri upendo wa Kristo ubadilishao na tumaini la Injili katika ulimwengu wa leo."