Theological Education - Signposts

NJIA YA KIANGLIKANA: ALAMA ZA SAFARI TUNAYOISAFIRI PAMOJA

Maandiko hayo  yanatokea baada ya mafautano  ya mikutano ya muda ya zaidi  ya miaka mine. Kati ya mikutano hio,   viongozi  wa  kanisa, wanatheologia na waalimu za  kitheologia  wamejitoa mno  watafakari juu ya mambo  ya kiAnglikana, yaani maana, maisha na matendo  ya  KiAnglikana. Wanafikiri mambo hayo  huitwa “Njia ya KiAnglikana” na kuwekwa kama msingi kwa kuelezea Uanglikana kwa maaskofu, wachungaji na walei.
Karatasi  hiyo  haiwezi kuelezea kila kitu cha Uanglikana, lakini inaweka alama zile zinazoonyeshea waAnglikana jinsi ya kutembea pamoja na wengine na kushirikiana nao wanapojitambua na kumfuata  Yesu Kristo.
Safari hii bado inaendeala kwa kuwa mazingira na hali tofauti hubadilishabadilisha maana ya Uanglikana. Katika historia ya kanisa aina tofauti za kiAnglikana zimeonekana mpaka sasa, na bado  zipo  kwenye ushirika wa KiAnglikana ya sasa hivi. Lakini waAnglikana wa kila aina hushirikiana vifaa  ya hali  moja vinavyowaunganisha ulimwenguni kote yaani “vifungo vya upendo” (bonds of affection). Alama zinazofuata chini huandikwa ili maana na utumishi wa kiAnglikana ujulikane vizuri zaidi na pia waAnglikana wote wafundishwe mno na kuwezeshwa kwa kumhudumia Mungu ujumbe wake  hapa duniani.

Njia ya Kianglikana ni njia moja inayoonyensha jinsi waKristo wanavyoishi katika Kanisa Takatifu, Katholiko na Apostoliko lililojengwa juu ya msingi  wa Bwana wetu Yesu Kristo. Njia hiyo

 • imepandwa juu na kutengenezwa na Maandiko Matakatifu;
 • pia imetunzwa na ibada zinazomheshimu Mungu anayeishi;
 • imejengwa kwa ushirikiano;
 • imefanya kanisa litoe ujumbe wa Mungu  hapa duniani kwa uaminifu .

Kila mahali tofauti ulimwenguni kote WaAnglikana  katika maisha yao  na matendo yao wanamshuhudia Bwana wetu aliyefanywa mwanadamu, akasulibiwa na akafufuka. Pia WaAnglikana wote huwezeshwa na Roho Mtakatifu kwa kazi hiyo.
Pamoja na Wakristo wote wenzao Waanglikana wanajitoa kuombea na kusubiri kwa hamu ufalme ujao wa Mungu.

Kutengenzwa na Maandiko Matakatifu

1 Sisi WaAnglikana husikiliza sauti ya Mungu anayeishi katika Maandiko  Matakatifu yaliyopokezanywa katika akili na mazoeo. Sisi  tunasoma Biblia, kila mmoja peke yake au pamoja:

 • tukitoa shukrani zetu kwa zamani zilizopita
 • tukijishughulisha na matendo yanayotokea sasa hivi
 • tukivumilia na kusubiri zamani zijazo kutoka kwa Mungu

2. Katika maisha yetu yote tunapenda mno Maandiko Matakatifu kila neno. Pia tunathamani Maandiko Matakatifu  yanavyotuonyesha jinsi  ya kumfuata Yesu kila mahali na kila hali. Sisi tunaomba na kuimba sifa zake katika ibada zetu na nyimbo  zetu. Orodha za masomo zinatufungulia baraka na neema za Maandiko Matakatifu kwa maisha yetu ya hapa duniani.

3. Tukijishusha na kujiweka chini ya mamlaka ya Maandiko Matakatifu sisi hufungiliwa mioyo yetu na masikio  yetu na kusikiliza vilevile.  Maandiko Matakatifu yametunzwa kama urithi wetu wa kiRoho, kwa mfano, katika Imani za Kanisa la kale, Kitabu cha Sala kwa Watu  Wote, na taratibu za Kanisa la KiAnglikana, yaani,

 • Sharti 39 za Dini za Kikristo,
 • Katekismo
 • Mkataba yenye Pembe Nne ya Lambeth (Lambeth Quadrilateral)

4. Tukihuburi na kumshudhudia Neno liliofanywa mwandamu, yaani, Yesu, pia tunawathamani waliosoma kwa taratibu na unagalifu Maandiko Matakatifu tangu  siku zile za kwanza mpaka sasa. Sisi pia tunaomba tuwe hivyo  tukiishi katika imani yetu, yaani, watu

 • tunaosoma na kujifunza pamoja
 • tunaosihi kati yetu kwa hekima, kwa nguvu, na kwa tumaini

Kila siku sisi twaona kwamba hali mpya zinaomba shauri mpya na majibu mapya yanayotokea kutoka maisha ya kiRoho na imani inayohusika na Maandiko Matakatifu.

Kutunzwa na Ibada

5. Mawasiliano yetu  na Mungu husaidiwa na jinsi tunavyokutana na Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu katika Neno na Sakramenti. Mazoeo hayo husaidia na kuongeza jinsi tunavyomjua Mungu na pia tunavyoshirikiana na waKristo wenzetu.

6. Kama waAnglikana tunamsifu Mungu, yaani Utatu Mtakatifu, tukisali pamoja na kupanga  ibada zetu katika uhuru na umoja. Tukitubu na kumshukuru Mungu tunajitoa na kumhudumia Mungu hapa duniani.

7. Katika ibada zetu na sala zetu sisi hujaribu  kuungunisha matokeo yenye maana kutoka zamani zilizopita pamoja na desturi na mira tofauti za jamii zetu mbalimbali za sasa hivi.

8.Sisi na jamii zetu tumesharibika na dhambi. Hata hivyo tunajua tunavyoomba msaada wa Mungu na  kusamehewa naye. Tunajua pia tunavyoishi katika neema na jinsi ya kutayarisha maisha yetu yawe safi mbele yake Mungu. Sisi tunavyosamehewa na Kristo na kuwezeshwa tuwe imara  katika neno na  sakramenti hutumwa tuingilie ulimwengu katika nguvu ya Roho Mtakatifu.

Kujengwa kwa Ushirikiano

9. Kwenye madayosisi na majimbo yetu yaliyoendeshwa na maaskofu na synodi sisi tumefurahi mno miito mbalimbali ya wote waliobatizwa. Kama ilivyoandikwa kwenye taratibu za kuweka wakfu  maaskofu, mashemasi na makasisi, vyeo hivi vitatu hufanya  wachungaji wahudumu ili waite watu wote wa Mungu  na kuwapangia na kuendeshea kazi  zao kama zilivyojulikana na kufanikiwa.

10. Sisi waAnglikana tunathamani mno tunavyoishi pamoja duniani  kote. Tunamweka Askofu Mkuu wa Canterbury awe mtu anayeonyesha alamu wa umoja wetu na kushirikiana pamoja na  Uaskofu wa Canterbury. Pia tunashika  vifaa vitatu kwa ushirikiano:

 • Mkutano wa Lambeth
 • Mkutano wa kushirikiana wa Kianglikana (Anglican Consultative Council)
 • Mkutano was Maaskofu Wakuu.

Mikutano hiyo mitatu pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury mwenyewe huunganisha  Ushirika wa KiAnglikana katika dunia bila kuweka mamlaka yote sehemu  moja peke: upendo  na vifungo  vyake  husaidia kazi zao vizuri zaidi.

11. Pia inabidi tukubali jinsi   jamii  za kimisionari na kimataifa (kwa mfano, UMAKI) jinsi  zinavyowasaidia kujenga umoja katika ushirika wetu.  Maisha tunayoyashirikiana katika ushirika wetu pia husaidiwa na kamati  mbalimbali, jamii tofauti, kazi tunazozishirikiana  na jirani zetu na vifungu vya undugu ( kwa mfano, kati ya madayosisi).

Kuendeshwa na Ujumbe wa Mungu

12.  Sisi waAnglikana twaitwa  tujitoe kwa ujumbe wa Mungu  hapa duniani. Sisi  tunafanya hivyo ktk kazi mbalimbali:

 • Kufundisha imani ya injili kwa upole na taratibu
 • Kusaidia wenzetu kwa upendo
 • Kutoa ushuhuda na unabii.

Tunapotoa ujumbe mahali petu mbalimbali sisi tunamhudumia na kumshuhudia Yesu Kristo Mwokozi wetu aliyesulibiwa na kufufuka. Tunamshangilia pia Mungu  alivyotusamehe na kutupa sisi uzima wa milele tukichungulia ushuhuda wenye gharama kubwa,imani na uaminifu uliotolewa na  wanawake, wanaume na watoto wa ushirika letu leo na tangu  zamani.

13. Pia tunakumbuka kwamba kazi zetu kwa ujumbe wa Mungu na maisha yetu ya kiKristo  hazifai  na hazitoshi. Zimechafuliwa na makosa mbalimbali:

 • Ubageuzi na ukoloni
 • Kutumia vibaya mamlaka na cheo
 • Kuweka pembeni kazi  za walei na wanawake
 • Kutotumia vizuri nguvu na vifaa na kutoshirikiana vizuri
 • Kushusha wamaskini na wale bile uwezo hekima yao.

Tukikumbuka makosa hayo tunaomba kujishusha na kubadilika ili  tumfuate Mungu kwa upole mpya na kushirikiana habari njema kwa furaha katika maneno yetu   na matendo  yetu tunavyojitoa.

14.  Tukisimama imara katika Kristo twashirikiana  na  watu wote wenye moyo safi katika kazi za kujengea amani, haki, upendo na msamaha ya Mungu. Tunajua shida kubwa ziko mbele ya sisi, kwa mfano:

 • Umaskini
 • Kutwalia Kanisa
 • Ubinafsi bila mwisho
 • Nguvu na ukali
 • Mateso ya waaminifu
 • Uharibifu wa mazingira
 • UKIMWI

Hatutakaa kimya mbele yao. Tutahubiri unabii kwa kuvunja falsafa  na visiasa vya udanganyifu na uharibifu. Pia tutaendelaa na mazoeo yetu mazuri kwa kuwasaidia watu ka njia za elimu, kiafya na uradhi.

15. Tukiwasiliana na watu wa dini  tofauti, tutamshuhudia  Bwana wetu Yesu Kristo katika amani, upole, akili na heshima.

16. Sisi WaAnglikana tunaobatizwa katika Kristo tunashirikiana na WaKristo  wenzetu wa madhehebu mbalimbali katika ujumbe wa Mungu. Tuna hamu sana kwa kuwasiliana vizuri na WaKristo wa madhehebu  tofauti. Mazoeo yetu  katholiko pamoja na yalivyotengenezwa ni baraka  kwa mawasiliano  wetu  na madhehebu mengine. Tunawasiliana  nayo kwa sababu tunaamini  na kutumaini kwamba WaKristo wote watashika umoja ule ambao Mungu ameshawapangia ili watu wote wa dunia wasikilize injili  ya Bwana wetu Yesu Kristo na kuiamini.

TEAC Anglican Way Consultation

Singapore

May 2007

 

Kiswahili  translation by Revd Dr Fergus King,
June 2007
To whom any errors should be attributed….