Mission - Commissions - IASCOME

Agano la Ushirika Katika Umisheni

Kiswahili

Tume ya Lambeth katika Windsor Report “ilipendekeza na kuwahimiza viongozi wa majimbo kufikiria jinsi makanis ya Ushirika wa Kianglikana, yatakavyochukua na kufuatilia Agano sawa, ambalo litaonyesha waziwazi na kwa dhati, uaminifu, na ushikamano wa upendo, unaoendeleza uhusiano kati ya makanisa ya ushirika.[1]

IASCOME imejadili njia za kutekeleza sehemu muhimu za umisheni katika Ushirika wa Kianglikana kufuatia miaka kumi ya uijilisti na harakati ya Washirika Umusheni. Wazo la Agano Katika UMission lililzuka kuwa kipengele cha mbele.  Twaamini ya kwamba Agano linaloshirikisha umuhimu wa umoja katika umisheni, lingeweza kuwa msingi wa husiano kati ya makanisa, mashirika ya umisheni na mitandao ya Ushirika huu zikatoa shabaha adhimu ya umoja katika umisheni kwa Ushirika wa Kianglikana (Anglican Communion).

Kwenye Maandiko, maagano ni muhimu hasa katika Agano La Kale kwa uhusano wa Mungu na Nuhu, Ibrahimu, Musa na uma wa Israeli. Jeremia na Ezekieli wanatabiri kuja kwa agano jipya- ambamo Mungu anawapa watu wake mioyo mipya na maisha mapya, naye atatembea nao, nao watatembea naye. Katika Agano Jipya, Yesu yuanzisha Agano hilo Jipya. Lilianzishwa na kuvunjwa kwa mwili wake na kumwagika kwa damu yake nalo lasherehekewa katika karamu muhimu ya Ushirika Utakatifu na kudhihirishwa kupitia Ufufuo wa Jesu Kristo kwa watu wote kwa nyakati zote.

IASCOME ilifikiria kwa undani Jinsi ya kubuni hulka ya agano. Tulitambua ya kwamba katika tamaduni zetu, agano ni makubaliano ya uzito na adhimu. Msingi wa maagano ni husiano ambamo watu hujitolea kwa hairi, hali mikataba yaweza kuwa mapatano ya kisheria chini ya Kanuni tawala. Maagano ni matoleo ya hairi mmoja kwa mwingine, hali mkataba unashikamanisha kwa utawala wa nje. Maagano ni ya kiuhusiano kati ya wanaofanya mapatano hayo na Kiuhusiano na Mungu na mbele ya Mungu.

Kwa vile sisi, Makanisa ya Kianglikana tuna desturi ya maagano yanayosaidia kufafanua uhusiano wetu na makanisa mengine, kwa mfano mapatano ya Porvoo kati ya Kanisa La Vingereza( Church of England) na makanisa ya Kilutheri eneo la bahari ya Baltic, na pia Wito kwa Umoja wa Umisheni, kati ya Kanisa la Episkopeli na Kanisa la uijilisti la kilutheri la Amerika.

Tunapendekeza kwa shauri ya ACC na majaribio ndani ya Ushirika, agano lifuatalo lenye vipengele tisa.Twaamini linatoa chanzo cha mapatano kati ya Makanisa ya Kianglikana  kitaifa – bali pia yaweza kutumiwa katika parokia/makanisa, mashirika na mitandao ya umisheni, wenzi kati ya madiyosisi n.k. Twaamini Agano kwa Ushirika wa Kianglikana katika umisheni unatoa mwelekeo wa kushikamanisha huu ushirika pamoja kwa hali tofauti na ile ya ‘The Windsor Report’.

Agano Kwa Ushirika Katika Umisheni

Agano hili la bainisha umoja wa mwito wetu kushiriki katika Kazi ya Mungu ya uponyaji na upatanisho kwa ulimwengu wetu uliobarikiwa walakini hali ya kuvunjika na wenye maumivu.

Katika uhusiano wetu kama ndugu na dada wa Kianglikana dani ya Kristo, tunaamini katika tumaini la umoja ambalo Mungu ameleta kupitia Yesu katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Utangulizi huu unatambua ya kwamba, Ulimwengu ni mmoja ulioneemeshwa na Mungu lakini Kazi ya Mungu kupitia Kristo, inayofulizwa na roho Mtakatifu, ni ya kutafuta kuponya daumivu ya dunia na kupatanisha matengano. Utangulizi huu, watukumbusha ya kwamba sisi wakristo tumeitwa kushirikisha husiano zetu katika umisheni wa Mungu ulimwenguni, tukishuhudia ufalme wa upendo, haki na furaha ulioanzishwa na Yesu Mwenyewe.

Tukijengwa na Maadika na Sakramenti tunajitolea kwa:

Vipengele tisa via agano vimesimama katika maandiko na sakramenti panapopatikana chakula rohoni, wongozi na nguvu za safari kwa wenzi agano pamoja

 1. Kutambua Yesu katika hali na maisha ya Kila Mmoja.
  Vipengele tisa viaanzo na  Yesu Kristo, chanzo na ufulizo wa imani yetu, na kutuelekeza kwa wale tunaopatana nao katika umisheni, kutafuta, kutambua na kujifunza kwao na kufurahia mbele za kazi ya kristo ndani ya maisha na hali za wenzetu.
 2. Kusaidiana Katika Kushiriki Kwetu Katika Kazi ya Mungu.
  Kipengele cha pili chatambua ya kwamba hatuwezi kutumika kwa kazi ya Mungu peke yetu na yahimiza kusaidiana, kujengana na kutiana moyo katika bidii zetu.
 3. Kukutana na Kushirikiana yanagotuungawisha na Kutafakari yanayo tugawanya.
  Kipengele cha nne chaelekeza kwa mikutano ya ana kwa ana ambamo mapya yaweza kushirikiwa na magumu kusawazishwa.
 4. Kuwa Tayari Kubadilika Wenzentu wanapo dhihirisha makosa kwetu.
  Kipengelecha tano chatambua ya kwamba chenga moto zinapotokea bas mabakiliko yatahitajika mamna ya wanafunzi wa Yesu unapokuwa kutokana na mapitoyetu katika umisheni na kukabiliand na wale tulio nao Agano.
 5. Kusherekea Nguvu zetu na kuomboleza unyonge wetu.
  Kipengele cha sita cha tuita kuheshimu na kusherekea tunayofaulu na kutambua fadhaa na unyonge wetu kwa tumaini la kurekebisha na kupatanishwa.
 6. Kushirikishana kwa usawa rasli mali Mungu alizotukirimia.
  Kipengele cha saba kinasisitiza ya kwamba kuna rasli mali za kugawana – sio pesa na watu tuu, bali mawazo, maolbi, uchangamfu, chengamoto, msisimko na kutuita kugawana rasli mali hizo hasa iwapo mmoja wa mshirki katika agano akiwa na zaidi ya  mwingine.
 7. Kufanya kazi pamoja Kustawisha viote alivyo viumba Mungu.
  Kipengele cha nane cha bainisha Mungu anavyojali alivyoviumba – sio binadamu tuu, bali vyote vilivyoumbwa – kwa hivyo twaitwa kufanya bidii kulinda vyote na kustawisha na kufanya upya maisha ya dunia.
 8. Kuishi na kuingia ndani ya ahadi ya Mungu ya Upatanisho wetu na wa ulimwengu.
  Kipengele cha mwisho chazungumza kuhusu tumaini la baadaye tunawishi kwalo, tumaini ya Ulimwengu – ambamo “mapenzi ya Mungu yatatimizwa duniani kama yalivyo mbinguni” ambavyo yesu alitufunza kuomba.

Tunafnya Agano hili kwa ahadi ya jukumu letu kwa kila mmoja na kutegemeana kuliko ndani ya Mwili wa Kristo.

Mwisho huu watukumbusha ya kwamba tunahitajiana, tuna jukumu mmoja kwa mwingine na tunategemeana katika Mwili wa Kristo.

IASCOME inapendekeza ya kwamba ACC iweke Agano la Ushirika Katika Umisheni ya Ushirika wa Kianglikana waliotunukiwa kuendelea Kuangalia maagano kwa niaba ya Ushirika, kama ilivyopendekezwa na Windsor Report na “Communique” ya Februari 2005 ya mkutano wa viongozi. Kumaliza, IASCOME inatoa makubaliano haya kubainishwa na ACC-13:

MAAZIMIO YA ACC-

Hii kamati:

 1. Yapendekeza Agano ya Ushirika katika umisheni kwa makanisa ya Ushirika wa Kianglikana kwa kuangalia na kutekeleza kama Maono ya uaminifu wa kianglikana kwa kazi ya Mungu.
 2. Yaendeleza Agano ya UshirIka Katika Umisheni Kwa Mashirika mbali mbali ya Kianglikana yaliyojukumishwa kuendelea kufikiria maagano kwa ushirika wa kianglikana kama ilivyo pendekezwa na Windsor Report na “Communique” ya mkutano wa viongozi Februari 2005.
 3. Inaachia Agano ya ushirika katika umisheni  kwa kongamano lijalo la Inter-Anglican Standing commission on Mission and Evangelism, kote katika Ushirika wa Kianglikana.

Agano limewakwa kwa ujumla makusudi. Katika kuelewa umisheni linajenga juu ya  vipengele Vitano Vya Umisheni vya 1984 na 1990 Anglican consultative Council.[2] Linatoa muelekeo ambamo wanaoingia waweza kuona na kuchagua kazi na  maelezo maalum yanayo fuatana na hali zao hususa.

[1] Windsor Report  pp. 62-64

[2] Kutangaza habari vyema ya ufalme wa Mungu; kufunza, kubatiza na kulea waamini wapya; kutumika katika mahitaji ya kibinadamu, kutafuta kubadilisha  hali zisizo haki katika jamii , kufanya bidii kulinda vyote alivyoviumba Mungu na kustawisha na kuboresha maisha ya dunia.